Global Learning

Yanga wamaliza mjadala wa Kakolanya kwa Staili hii


Wakati hatma ya Beno Kakolanya ndani ya Yanga ikiwa bado haifahamiki kutokana na kile ambacho kimekuwa kikiendelea kati yao, Yanga wakidai hawajui alipo Beno Kakolanya na Kipa huyo akiwa bado haonekani mazoezini wala kambini.


Klabu ya Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa kamati ya mashindano na usajili Hussein Nyika imesema kuwa wao kama Yanga wanatambua kuwa bado Beno Kakolanya ni mchezaji wao
Lakini hawajui yupo wapi maana alipoondoka hakutoa taarifa na wao kama uongozi wanachosubiri ni kumuuliza alikuwa wapi kwa siku zote ambazo hakuwa kambini na kuhudhuria mazoezi.
Nyika  alienda mbali kwa kusema kuwa hawawezi kumtafuta Beno Kakolanya kumuuliza yuko wapi kwasasa kwani hiyo si kazi yao bali Beno ndiye anayetakiwa atoe taarifa juu ya wapi alipo na kwanini haonekani katika programs zinazoendelea ndani ya yanga.

Walichokisema Yanga baada ya tetesi za Kumrejesha Niyonzima dirisha dogo


Walichokisema Yanga baada ya tetesi za Kumrejesha Niyonzima dirisha dogo
Siku za Karibuni kumekuwa na tetesi nyingi zikiwahusisha baadhi ya wachezaji kutua Yanga wakati wa Dirisha dogo la Usajili TPL msimu wa 2018/2019.


Moja kati ya tetesi ambayo imekuwa ikichukua nafasi imekuwa ikimhusisha mchezaji wa zamani wa Yanga anayekipiga kwa sasa katika klabu ya Simba Haruna Niyonzima kuelezwa anaweza kutua Yanga wakati huu wa Dirisha Dogo.
Uongozi wa Klabu ya Yanga msomaji wa Kwataunit.co.ke kupitia kwa Afisa habari wake Dismas Ten umeeleza kitu kuhusiana na tetesi za Yanga kuhusishwa katika sakata la usajili wa Haruna Niyonzima.


Baada ya kuulizwa kuhusu habari za Yanga na Niyonzima Ten amefunguka kuwa watu wasubiri mpaka tarehe 15 December kila kitu wataweka wazi lakini pia Ten hakusita kumsifia Haruna Niyonzima kwa kusema kuwa bado anauwezo mkubwa lakini habari za Usajili wake watu wasubiri tarehe 15 December kila kitu na wachezaji waliosajiliwa watawekwa wazi.

Breaking News: Zahera amaliza kila kitu usajili wa Boban Yanga


Wakati watu wakiwa bado wanajiuliza kuhusiana na usajili wa mchezaji wa African Lyon Haruna Moshi Boban Kutua Yanga na mvutano ukiwa kama anafaa au  hafai Zahera amemaliza kila kitu.
Akizungumzia kuhusu mchezaji Hugo Mwinyi Zahera amefunguka kuwa yeye alimuona Boban alipokwenda kwa moja ya wadau wakubwa wa Yanga Ndama 
Akiwa ofisini kwa Ndama kulikuwa na mchezo ukiwahuusisha African Lyon na baada ya   kuona uwezo wake alipendezwa Naye na akamwambia Ndama.
Kwahiyo usajili wa Haruna Moshi Boban ni pendekezo LA kocha mwenyewe Mwinyi Zahera

Simba level Nyingine Straika wa kiwango cha Kimataifa anatua

Simba level Nyingine Straika wa kiwango cha Kimataifa anatua

Hii Simba hakika haijapanga kufanya vizuri tu katika ligi kuu soka ya Tanzania bara bali ni katika michuano yote ambayo itakuwa ikishiriki ndani na nje ya Nchi.

Wakati kocha Mkuu wa Klabu ya Simba akiendelea kusisitiza kuwa bado hajamaliza usajili wake licha ya Kuongeza beki mmoja kumrithi Kapombe ambaye aliumia akiwa na timu ya taifa.

Kocha Aussems alisisitiza kuwa bado ataongeza mchezaji mmoja licha ya kutofunguka ni mchezaji gani wala nafasi gani anataka kuongeza.


Habari za kuaminika ambazo kwataunit.co.ke imezipata inaelezwa kuwa Simba wameingia kwenye rada za kuinasa saini ya Straika wa AS Vita ya Congo JM Makusu Mundele.

Mundele  ni moja ya wachezaji tegemeo katika timu ya AS Vita ya Congo akiisaidia msimu huu kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika CAF.

Walichokisema Yanga baada ya Tetesi za Haruna Moshi kusajiliwa
Inaelezwa Kuwa Simba wameamua kufanya namna ya Kumpata Straika huyo kwani mshambuliaji wao Emmanuel Okwi inaelezwa anaweza kutimkia Afrika Kusini mwezi January katika klabu ya Kaizer Chief.

Usajili Simba: Mashine mpya inatua kabla ya dirisha kufungwa Aussems afunguka

Kocha Mkuu wa klabu ya Simba Mbelgiji Patrick Aussems amefunguka mengi kuhusiana na usajili kwenye kikosi chake cha Simba kabla ya
Tunahitaji mchezaji mpya na tutamsaini kabla ya dirisha dogo kufungwa Jumamosi 15 December 2018, Uongozi unakamilisha masuala yote na ndani ya saa 48 kila kitu kitakuwa sawa.
Kuhusu anatokea wapi na nafasi yake.?
Kocha Patrick Aussems ambaye amekiri kuwa akili kubwa kwasasa ipo kwenye mchezo dhidi ya Nkana Fc Jumamosi 15 December amefunguka kuwa mchezaji huyo huenda akawa kiungo, au mshambuliaji au hata nafasi nyingine


Na Kuhusu anatokea wapi hakutaka kusema alisihia kusema tu kuwa anaweza akawa wa ndani au wa Nje ya Nchi lakini kila kitu kitakaa sawa ndani ya masaa 48 yani siku 2 hizi.
” Inawezekana akawa mchezaji wa ndani au wa nje inawezekana akawa anacheza nafasi ya kiungo au msjhambuliaji wa hata nafasi nyingine lakini tutakamilisha ndani ya saa 48″
Akizungumzia kuhusu hali ya kapombe kocha Aussems msomaji wa Kwataunit.co.ke amefunguka kuwa mchezaji huyo ni muhimu sana na wanamuombea apone haraka ili aweze kukitumikia kikosi cha Simba
Kuhusu Beki Zana Coulibaly Aussems ameweka wazi kuwa kinachosubiriwa ni ITC yake na Baadhi ya vibali vya kumuwezesha kuanza kufanya kazi.

Habari mpya kutoka Simba leo 11 December 2018


Klabu ya Simba leo 11 December 2018 imetoa Taarifa mpya kuelekea mchezo wao dhidi ya Nkana Fc mchezo utakaochezwa huko Kitwe nchini Zambia.
Klabu ya Simba imeandika kuhusiana na washabiki wanaotaka kwenda kuisapoti timu yao kwenye mchezo huo wa ugenini klabu bingwa barani Afrika.
katika Ujumbe ulioandikwa na Simba leo ndiyo siku ya mwisho kwa wanaotaka kujiandikisha kwenda.

Winga mkongo azuiwa mazoezini Yanga

KATIKA hali ya kushangaza, juzi Jumamosi, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera alimzuia kiungo mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Ruben Bomba kukanyaga kwenye mazoezi ya timu hiyo.

Bomba, raia wa DR Congo, anayetokea kwenye akademi ya Azizi Makukula, aliyechezea timu ya taifa ya Ureno, yupo nchini kwa ajili ya kujiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo utakaofungwa Desemba 15, mwaka huu.

Akizungumza nasi  Zahera alisema kuwa licha ya mchezaji huyo kufanya mazoezi siku moja, lakini aliamua kumsimamisha kwa kuwa hakutaka kuvuruga mipango yake.
“Bomba amefanya mazoezi na sisi siku moja ya Ijumaa lakini leo (juzi) hakuweza kufanya kwa sababu nilizuia yeye kuja mazoezini kwa kuwa hakuwa kwenye mipango ya mechi yetu na Biashara United.

“Unajua bado yupo kwenye mazungumzo na uongozi halafu wakati anakuja sisi tulienda Mbeya, hivyo hata mazoezi ya siku moja aliyofanya hayawezi kutoa ubora wake na tulifanya sana fiziki kuliko kuchezea mpira ila mazoezi yanayofuata atakuwepo,” alisema Zahera.
source : Champion
Older Posts
© Copyright Global Learning Published.. Blogger Templates
Back To Top