Zahera Afunguka siri ya Ushindi Yanga | Global Learning

Zahera Afunguka siri ya Ushindi Yanga

BAADA ya maswali lukuki kutoka kwa wapenzi wa soka nchini wanaohoji kasi ya Yanga katika mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara wakati klabu hiyo ikielezwa kukabiliwa na ukata, hatimaye siri ya mafanikio hayo ya wakali hao wa Jangwani imefahamika, huku ‘sterling’ (nyota) akiwa ni Kocha Mkuu wao, Mwinyi Zahera.


Tangu msimu huu wa Ligi Kuu Bara ulipokuwa ukianza, Yanga haikuwa ikipewa nafasi ya kufanya vizuri kwa kuwa hawakufanya usajili wa kishindo kama ilivyokuwa kwa watani wao wa jadi, Simba na Azam.
Katika dirisha kubwa la usajili kabla ya kuanza kwa ligi, Yanga ilishindwa hata kusajili wachezaji wa ndani waliong’ara kutokana na kukosa fedha za kufanikisha mchakato huo.


Lakini mara baada ya kuanza kwa ligi hiyo, Yanga imejikuta ikiwa tishio, ikishinda mechi 13 kati ya 13, huku ikipata sare mbili tu hivyo kujikusanyia pointi 41 na hivyo kukaa kileleni mwa kipute hicho.
Wakati wapenzi wa soka nchini wakiwa bado wanajiuliza juu ya kasi hiyo ya Yanga, Zahera amefichua kilicho nyuma ya pazia akisema mbali ya maelekezo yake na jitihada za wachezaji, lakini amekuwa akiwapandisha mzuka vijana wake kwa kuwapa ‘zawadi’ kila wanaposhinda.
Akizungumza na nasi juzi baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Biashara United kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Zahera alisema wanapokuwa mapumziko ana kawaida ya kuwaahidi wachezaji wake kuwapa zawadi ili kuwapa mzuka wa kupigana kiume kuipa ushindi timu yao.
“Huwa ninawaambia kuwa mnatakiwa kuingiza goli la kwanza, la pili na tunatakiwa kushinda na wakifanikiwa ninawapa zawadi. Huu mtindo huwa unatumiwa sana na makocha wengi, hata wa Ulaya. Mfano Jose Morinho,” alisema Zahera.
Alifafanua kuwa tayari wachezaji wake wameshazoea hali hiyo na ndio sababu ya matokeo wanayopata na amefanya hivyo pia katika mechi ya juzi dhidi ya Biashara United.
Licha ya Zahera kutoweka wazi zawadi anazowapa wachezaji wake, lakini mmoja wa nyota wa Yanga ameliambia BINGWA kuwa kocha huyo huwa anawapa fedha kuanzia 50,000 hadi 100,000 pale wanapofanikiwa kufanya vile anavyotaka.
“Kocha tukishamaliza mechi anatuambia mmefanya vizuri sana, nawapa zawadi, ndio anatupatia hela, kuna mechi nyingi anafanya hivyo, ndio maana hata tunapokuwa tumeanza kufungwa kipindi cha pili lazima turudishe na kuongeza ya ushindi baada ya kocha kutuahidi zawadi, huyu mwalimu ni kama mzazi na rafiki yetu, anajua sana kuishi na wachezaji kwa upendo,” alisema mchezaji huyo.
Katika hatua nyingine, Zahera amemsifia nahodha wa timu hiyo, Kelvin Yondani,  kuwa ni moja ya mabeki wenye akili nyingi, akisisitiza iwapo angekuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi ya kutosha kila siku, angekuwa akitamba katika ligi kubwa za Ulaya.
“Yondani ni beki mwenye akili sana Tanzania, anafanya kazi kubwa sana uwanjani na majukumu yake ya unahodha anayamudu, anastahili pongezi,” anasema.
Katika mechi za hivi karibuni, Yanga imekuwa ikianza kufungwa kipindi cha kwanza lakini wanaporejea cha pili, wanakuwa tofauti na kurejesha na hatimaye kupata ya ushindi.
source : Bingwa
▼▼▼BOFYA PICHA HAPA CHINI KUONA VIDEO HIYO ▼▼▼
“In fact, all the leaders I met in the UAE praised us for maintaining peace, a prerequisite to achievement in development,” Dr Shein said at the press conference held at the airport in Zanzibar shortly after landing from the Arab countries. On January 21, this year the President and his delegation which included First Lady Mwanamwema Shein left the Islands for a week-long visit in countries forming UAE: Dubai, Sharjah, and Ras-al- Khaimah. He said the reception he was accorded in each state was good, and that leaders in the Arab countries had promised to support Zanzibar move ahead in various sectors, including the search for alternative energy, oil and other natural resources, improvement of social services and infrastructure. Dr Shein said, “… I personally learned a lot. The countries are economically well-off, but they have managed to advance because of determination and good planning, tools which we (Zanzibar) can copy from them.” He said without good planning, even if you have money, one can fail to move forward as witnessed in some countries including in Africa where some nations have good economy, but have failed to achieve development goals. Speaking with Journalists, the isles leader also answered questions which were not directly related to his trip. When asked to comment on ongoing views about changing presidential term limit from the current five to seven, he replied “It is not my agenda; I will respect my constitution term and leave the office to others.” He was also asked about the temporary ban on registration of international ships after some foreign ship flying Tanzania flag were implicated in illegal business, he said “I know there are discussions going on. It is the dishonest ships abroad are to blame for misusing our flag. I hope we will have the right to continue registering international ships.”

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright Global Learning Published.. Blogger Templates
Back To Top